Michezo MingineTennis

Gauff kumvaa Sabalenka fainali US Open

KINDA Coco Gauff ametinga fainali ya michuano ya wazi ya tenisi ya Marekani(US Open) kwa mchezaji mmoja mmoja kwa mara ya kwanza baada ya kumtoa Karolina Muchova katika nusu fainali iliyogubikwa na waandamanaji wanaopinga uharibifu wa mazingira.

Gauff raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 19 alikamilisha ushindi dhidi ya Muchova wa Jamhuri ya Czech anayeshika namba 10 duniani kwa seti 6-4 7-5 waliporejea baada ya mchezo kuchelewa kwa dakika 49.

“Nilikuwa naangalia mashindano haya tangu nikiwa mdogo, ninahisi ni ya kipekee sana. Lakini kazi haijakamilika,” amesema Gauff.

Gauff anayeshika namba 4 duniani kwa mchezaji mmoja mmoja atamkabili Aryna Sabalenka anayeshika namba 2 katika fainali itakayopigwa Septemba 9 kwenye uwanja wa tenisi wa Arthur Ashe jijini New York.

Related Articles

Back to top button