Al Ahly wapewa ‘kosta’ Kenya
NAIROBI: Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani Afrika Al Ahly wamewasili jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wa kwa wa raundi ya pili ya hatua za awali za michuano hiyo dhidi ya wenyeji wao Gor Mahia.
Al Ahly walitua nchini humo jana majira ya saa 3 za usiku kisha kukutana na mapokezi ambayo vyombo vya habari nchini kenya vinaripoti hawakuyapenda.
Wenyeji wao Gor Mahia waliwaandalia basi dogo aina ya Toyota Coaster ili mabingwa hao wa Afrika watumie kuelekea hotelini kutoka airport kitendo ambacho wadau wengi wa soka nchini Kenya wameona ni kuwakosea heshima.
Gor Mahia na Al Ahly watakiwasha kesho Septemba 15 majina ya saa 9 alasiri saa za Afrika Mashariki katika dimba la Nyayo jijini Nairobi.
Mara ya mwisho kwa Gor Mahia kucheza na timu kutoka nchini Egypt ni mwaka 2019 Mabingwa hao wa Kenya wakiichakaza Zamalek ya Egypt mabao 4-2
Gor Mahia wanakutana na Ahly baada ya ushindi mnono wa 5-2 mbele ya Al Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini huku Ahly akisubiri mshindi wa mechi hiyo katika raundi ya pili ya hatua za awali za michuano ya klabu bingwa barani Afrika.