Taji Liundi: Natamani ‘Komasava’ impatie pesa nyingi Diamond
DAR ES SALAAM: MTANGAZAJI Taji Liundi anatamani mafanikio anayopata msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupitia wimbo wake wa Komasava yasiishie kwenye kuchezwa na wasanii wa kimataifa tu bali uwe sehemu ya kumuongezea kipato kwa kupata shoo nyingi.
Akizungumza na Spotileo, Taji amesema kuwa watu wanafurahia kuwa wimbo umefika mbali tuombee apate na shoo ili zimuingizie kipato.
“Wimbo umefanya vizuri tumeona umechezwa na wasanii wakubwa ikiwepo Chris Brown ni vizuri baada ya hapo nini kinafata inahutajika kuona mafanikio zaidi kuwa wimbo umeingiza shoo nyingi kiasi gani? Binafsi natamani aingize mapato zaidi,” alieleza Taji.
“Mafanikio ya kitu yanaendana na faida aliyoingiza kwa kupata shoo au malipo yaliyopa kwenye wimbo uliofanyika tunafurahi nyimbo zetu zinapofanya vizuri na mafanikio yawepo.