Muziki
Miaka 20 ya Christan Bella usipime!

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa dansi Christian Bella kesho anatarajia kufanya tamasha maalum la kuadhimisha miaka 20 ya safari yake ya muziki, litakalofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.
Tamasha hilo linafanyika kama sehemu ya shukrani kwa Watanzania kwa sapoti kubwa waliompa katika kazi yake ya muziki, pamoja na kushukuru baada ya kupewa rasmi uraia wa Tanzania.
Akizungumza na Spoti leo Bella amesema kuwa akiwa sasa ni Mtanzania kamili, anaona fahari kusherehekea pamoja na mashabiki wake kwa kuwapatia burudani ya nguvu na show ya kukata na shoka ambayo haitakiwi kukoswa.
Mashabiki wengi wanatarajia kusikia nyimbo zake maarufu zilizotikisa kwa miaka mingi na kufanya usiku huo kuwa wa kipekee zaidi.




