EPL

Man United kujenga uwanja mpya

Utakuwa na uwezo wa kubeba watu laki 1

MANCHESTER:UONGOZI wa klabu ya Manchester United, kupitia bilionea wake Sir Jim Ratcliffe, umetangaza mpango wa kujenga uwanja mpya wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 100,000, jirani na uwanja wao wa sasa wa Old Trafford. Uwanja huo unatarajiwa kuwa moja ya viwanja vikubwa zaidi barani Ulaya.

Awali, bilionea huyo aliweka wazi matamanio yake ya kuona klabu hiyo inakuwa na uwanja mkubwa na wa kisasa tangu alipotwaa hisa za umiliki wa klabu hiyo mwezi Februari mwaka jana.

“Leo ni mwanzo wa safari adhimu ya kuwasilisha kile kitakachoweza kuwa uwanja mkubwa zaidi wa kandanda ulimwenguni, katikati mwa eneo letu pendwa la Old Trafford lililojengwa upya,” alinukuliwa Jim Ratcliffe katika taarifa ya Manchester United.

United tayari imezindua michoro ya usanifu wa uwanja huo mpya katika hafla iliyofanyika leo Jumanne asubuhi jijini London.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button