Ligi Kuu

Singida Black Stars kazi imeanza

KLABU ya Singida Black Stars imeshindwa kutamba nyumbani kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa CCM Liti Singida.

Singida Black Stars walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji Elvis Rupia dakika ya 14 na kisha baadaye Wilson Nangu akaisawazishia JKT dakika ya 67 ya mchezo.

Dakika ya 45 kipindi cha kwanza mchezaji wa JKT Tanzania  Hassan Dilunga  alikosa mkwaju wa penalti na kuufanya mchezo huo Kwenda mapunziko Black Stars wakiwa kifua mbele. Golikipa wa Black Stars Metacha Manta ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kuokoa michomo kadhaa.

Huu ni mchezo wa kwanza Black Stars wanashindwa kupata ushindi baada ya kutamba kwenye michezo minne mfululizo ya Ligi Kuu.

Matajiri hao wa Singida wamefikisha pointi 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu sawa na Fountain Gate FC.

Related Articles

Back to top button