Ligi KuuNyumbani

Azam kuendeleza ubabe Ligi Kuu?

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu kufanyika Kagera, Geita na Mbeya.

Vinara wa ligi, Azam yenye pointi 28 baada ya michezo 12 ipo ugenini dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kagera Sugar inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 12.

Mkoani Mbeya, maafande wa Tanzania Prisons inayoshika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 13 itakuwa mwenyeji wa Namungo iliyopo nafasi ya nane ikiwa na pointi 17.

Singida Fountain Gate inayoshika nafasi ya nne ikiwa na pointi 20 baada ya michezo 13 itakuwa mgeni wa Geita Gold iliyopo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 12.

Related Articles

Back to top button