KLABU ya Mashujaa ya Kigoma inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara imetangaza kumsajili kiungo Balama Mapinduzi.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Mashujaa imesema: “Tumekamilisha usajili wa fundi wa mpira Balama Mapinduzi @officialbalama rasmi yupo tayari kuwatumikia Watanganyika.”
Balama amejiunga na Mashujaa akitokea Mtibwa Sugar aliyojiunga nayo Agosti 2022 akitokea Yanga.