Wasifu

Mario Zagallo afariki dunia

GWIJI wa mpira wa miguu wa Brazil, Mario Zagallo ambaye alishinda Kombe la Dunia mara nne akiwa mchezaji na kocha amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.

Zagallo alikuwa winga katika timu ya taifa ya Brazil ambaye alishinda Kombe la Dunia mfululizo mwaka 1958 na 1962 akianza katika kikosi cha kwanza fainali zote mbili.

Aliiongoza timu ya taifa inayofikiriwa kuwa bora zaidi ya kimataifa ya wakati wote akiwemo Pele, Jairznho na Carlos Alberto kushinda Kombe la Dunia mwka 1970.

Kwa mara ya mwisho Zagallo alishinda fainali za Kombe la Dunia akiwa kocha msadizi wa Carlos Alberto Parreira mwaka 1994.

Zagallo alikuwa mtu wa kwanza kushinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji na Kocha.

Ukurasa rasmi wa Instagram wa Zagallo umesema una huzuni kubwa kutangaza kifo hicho.

“Alikuwa baba aliyejitolea, babu mwenye upendo, baba mkwe anayejali, rafiki mwaminifu, mtaalamu aliyeshinda na mwanadamu mkubwa. Mfano mkubwa. Mzalendo anayetuachia urithi wa mafanikio makubwa,” imesema taarifa ya ukurasa huo.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Brazil (CBF) Ednaldo Rodrigues amesema: “CBF na soka la Brazil wanaomboleza kifo cha mmoja wa magwiji wake.”

Mke wa Zagallo aliyekuwa na umri wa miaka 57, Alcina de Castro alifariki dunia mwaka 2012. Walijaliwa kupata watoto wanne.

Related Articles

Back to top button