Wasifu

Santos yashuka daraja baada ya miaka 111

KLABU ya zamani ya gwiji wa Brazil, Edson Arantes do Nascimento maarufu ‘Pele’ imeshuka daraja kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 111 ya timu hiyo.

Imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu ya Brazil, Seria A baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Fortaleza kwenye uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wa mwisho wa ligi wa msimu.

Santos ilitwaa mataji 12 ya taifa, sita ya ligi na mawili ya Copas Libertadores miaka ya 1950 na 60 wakati huo ikiwa moto wa kuotea mbali.

Pele aliyehusika kutwaa Kombe la Dunia mara tatu akiwa na timu ya taifa ya Brazil alifariki dunia mwaka jana akiwa na umri wa miaka 82.

Santos ambayo pia ametoka mfungaji bora wa muda wote Brazil, Neymar imekumbwa na tatizo la masuala ya kiuchumi katika miaka ya hivi karibuni.

Flamengo na Sao Paulo ndizo klabu pekee zilizosalia katika Ligi Kuu ya Brazil ambazo hazijawahi kushuka daraja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button