Wasifu

Yaya Toure aula Saudi Arabia

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu (SAFF) Saudi Arabia limemteua kiungo wa zamani wa Ivory Coast, Yaya Toure kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 40 atafanya kazi pamoja na Roberto Mancini ambaye alikuwa kocha wake katika klabu ya Manchester City.

Toure, ambaye amecheza City kwa miaka nane baada ya kusaini mwaka 2010, alianza ukocha mwaka 2019 na anaacha majukumu yake katika klabu ya Standard Liege ya Ubelgiji.

Kiungo huyo wa zamani wa Barcelona pia amezitumikia Donetsk Olympic ya Ukraine, Grozny ya Urusi na kama kocha wa kituo cha kukuza vipaji vya mpira wa miguu katika klabu ya Tottenham Hotspur.

wakati akisakata kabumbu Toure alicheza michezo 101 timu ya taifa ya Ivory Coast, akishinda kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 na pia mataji 18 katika klabu alizocheza Ugiriki, Hispania, England na China.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button