Tetesi

Tetesi za usajili Ulaya

BAYERN München inapanga kuwasilisha ofa ya pili kwa Tottenham Hotspur kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa England, Harry Kane. (Sky Sport)

Bingwa wa England, Manchester City inajiandaa kupeleka ofa kwa ajili ya kumsajili beki wa Croatia, Josko Gvardiol mwenye umri wa miaka 21, baada ya kuanza mazungumzo rasmi na RB Leipzig. (ESPN)

Kiungo wa Liverpool, Jordan Henderson, (33) na mshambuliaji wa Chelsea, Pierre Aubameyang (34) wapo kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na Al Ettifaq ya Saudi Arabia baada ya klabu hiyo kumteua Steven Gerrard kuwa kocha mkuu. (Mail).

Paris Saint-Germain inapanga kuzivuruga Chelsea, Liverpool na Manchester City katika usajili wa kiungo wa Celta Vigo ya Hispania, Gabri Veiga(21). (The Guardian).

Liverpool imepiga hatua kadhaa katika mbio za kumsajili kiungo Romeo Lavia wakati huohuo imeripotiwa klabu hiyo inapanga kuwasilisha ofa yao ya kwanza. Southampton wanataka pauni milioni 50. (Talksport).

Katika hatua nyingine Arsenal iko tayari kufanya usajili wa kiungo Lavia kutoka Soton na itakamilisha dili hilo mara baada ya kumalisha usajili wa Declan Rice. (Times – subscription required)

Manchester United inakaribia kumpa mkataba mpya mshambuliaji Marcus Rashford, wakati huohuo inaendelea na mipango ya kumnasa mshambuliaji Randal Kolo Muani kutoka Eintracht Frankfurt(24). (CBS)

Imeandaliwa na Rahim Fadhili

Related Articles

Back to top button