Tetesi

Calafiori bado kidogo Arsenal

ARSENAL inakaribia kunasa saini ya beki wa Bologna, Riccardo Calafiori.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari kutoka nchini Italia, Fabrizio Romano, Arsenal imetuma ofa mpya ya €50m saa chache zilizopita. Ofa hiyo inajumuisha add-ons na sell-on clause.

Romano amesema majadiliano baina ya Arsenal na Bologna yapo katika hatua za mwisho pia wakala wa mchezaji huyo Lucci yupo kwenye mazungumzo hayo.

Calafiori amekubali kujiunga Arsenal kwa mkataba wa miaka mitano mpaka 2029 na sasa anasubiri hatma ya mazungumzo yanayoendelea.

Endapo Calafiori atajiunga na timu hiyo utakuwa usajili wa kwanza Emirates kwa msimu huu. Beki huyo raia wa Italia ana uwezo wa kucheza beki wa kati, lakini pia beki wa kulia.

Related Articles

Back to top button