Suarez kukiwasha Inter Miami
TETESI za usajili zinasema fowadi wa Uruguay na Gremio, Luis Suarez, mwenye umri wa miaka 36 anatarajiwa kujiunga na Inter Miami ya Marekani mwaka 2024.
Atajiunga tena na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona Lionel Messi, Sergio Busquets na Jordi Alba.(El Pais – in Spanish)
Chelsea na Arsenal zote zina nia kumsajili Ivan Toney baada ya Brentford ‘The Bees’ kuthibitisha itamuuza fowado huyo wa England mwenye umri wa miaka 27 kwa bei sahihi.(Express)
The Bess imesema Toney ana thamani ya pauni milioni 100 lakini inakusudia kumbakisha hadi mwisho wa msimu huu.(Sky Sports)
Real Madrid itashindana na Liverpool na Manchester United kuwania saini ya beki wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Goncalo Inacio mwenye umri wa miaka 22.(AS – in Spanish)
Newcastle United ina nia kumsajili kiungo wa kihispania Gabri Veiga mwenye umri wa miaka 21, ambaye alijiunga na Al-Ahli ya Saudi Arabia kutoka Celta Vigo majira yaliyopita ya kiangazi.(Fichajes – in Spanish)