Tetesi

Al Nassr mikono juu kwa Mitoma

BRIGHTON: Matajiri wa Saudi Pro League Al Nassr FC wamesitisha rasmi majaribio ya kumsajili winga wa Brighton Kaoru Mitoma baada ya klabu yake hiyo kukataa dau la Euro milioni 65 huku wakitarajia dau kubwa zaidi.

BBC sport imeripoti kuwa katika mazungumzo zaidi baina ya klabu hizo Brighton waliweka wazi kuwa mchezaji huyo mwenye 27 hauzwi na hawako tayari kubadili msimamo wao juu ya kumbakiza hata iweje jambo lililopelekea Al Nassr kukubali yaishe.

Mitoma amecheza michezo 92 tangu awasili Amex stadium kutoka Kawasaki Frontale ya ligi kuu ya Japan J-league mwaka 2021 na tayari akiwa amecheka na nyavu mara 18

Mjapani huyo anasalia mchezaji pekee wa Brighton kucheza michezo yote 23 ya ligi kuu ya England huku kikosi hicho cha Fabian Hurzeler kikikamatilia nafasi ya 9 kwenye ligi. Mitoma aliongeza mkataba wa kuendelea na klabu hiyo hadi mwaka 2027 mwezi Oktoba mwaka 2023.

Related Articles

Back to top button