EPLKwingineko

Dyche kuwa kocha mpya Everton

Sean Dyche anatarajiwa kuteuliwa kocha mpya wa Everton ‘The Toffees’ kuchukua nafasi ya Frank Lampard aliyetimuliwa kazi Januari 24.

Dyche na kocha wa zamani wa Leeds United Marcelo Bielsa walikuwa washindani wakuu wawili baada ya kuwa na mazungumzo na uongozi wa Everton.

The Toffees inataka kuwa na kocha mpya kabla ya mwisho wa wiki hii.

Mazungumzo ya Bielsa na Everton hayakuleta matokeo yoyote hivyo Dyche mwenye umri wa miaka 51 kubaki chaguo pekee ingawa haijafahamika mkataba wake utakuwa wa muda gani.

Everton inayoshika nafasi ya 19 katika msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) itashuka uwanja wake wa nyumbani wa Goodison Park Februari 4 kuwakabili vinara wa ligi hiyo, Arsenal.

Related Articles

Back to top button