KwinginekoSerie A

Leao katika rada za Liverpool, Chelsea

KLABU za Liverpool na Chelsea zinavutiwa na fowadi wa AC Milan, Rafael Leao na huku ikiwa imesalia miezi 18 kwenye mkataba wake, zinapima kufikia kifungu chake kikubwa cha kuachiliwa.

Ripoti zimesema Leao amehusishwa kuondoka Milan kufuatia mwanzo mzuri wa msimu akiwa na klabu hiyo ya Italia.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amefunga magoli tisa na kusaidia 10 katika michezo 32 aliyocheza hadi sasa msimu wa 2022/23.

AC Milan imesema Leao ana kifungu cha kuachiliwa cha pauni milioni 131.9 sawa na shilingi bilioni 369.6 katika mkataba wake unaoishia Juni 2024.

Related Articles

Back to top button