Muziki

Jay-Z ajichagua mwenyewe kutumbuiza Super Bowl

NEW YORK: RAPA Jay-Z ambaye ndiye mtoa maamuzi mkuu kuhusu nani atatumbuiza kila mwaka kwenye Super Bowl, inasemekana amejichagua mwenyewe kutumbuiza kwenye hafla hiyo msimu huu!

Mtandao wa Puck News umeripoti kuwa gwiji huyo alitumia wiki kadhaa kutafakari anayefaa kupanda jukwaani katika tukio hilo kubwa la michezo, na hatimaye akaamua kuwa yeye ndiye mtu sahihi zaidi.

Pia, vyanzo mbalimbali vimefunguka kuwa uamuzi wa Jay kujichagua mwenyewe ulionekana kuwa wazo ‘lenye mvuto zaidi’ kuliko kumchagua Miley Cyrus au Justin Bieber.

Wawili hao ndio walionekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuchaguliwa kwa ajili ya Super Bowl LXI ambayo msimu huu itafanyika Uwanja wa SoFi mnamo Februari 14, mwakani.

Licha ya taarifa hiyo, hakuna tangazo rasmi lililotolewa kuhusiana na Super Bowl na Mtandao wa TMZ uliwasiliana na uongozi wa Roc Nation, lakini haukupata majibu yoyote.

Mwaka 2019, Kampuni ya Jay-Z, Roc Nation, iliripotiwa kupata mkataba wa Dola milioni 5 kwa mwaka kwa ajili ya kuandaa maonesho ya kipindi cha mapumziko na kampuni hiyo iliongeza mkataba huo mwaka 2024 kwa miaka mitano mingine.

Related Articles

Back to top button