Muziki

Mastaa Afrika kuwania Billboard 2024

LONDON: WANAMUZIKI Burna Boy, Tyla, Asake na Tems wameteuliwa kuwania Tuzo za Muziki za Billboard 2024, zinazoangazia kuimarika kwa muziki wa Kiafrika.

Katika tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Desemba 12 mwaka huu kwa afrika, mwanamuziki Tems ameng’ara zaidi kupitia wimbo wake maarufu wa ‘Me & U’ akiwa katika vipengele vitatu.

Mwanamuziki Taylor Swift ndiye ameongoza kwa wasanii wote akiwa ameteuliwa katika vipengele 16 kikiwemo ‘Msanii Bora’ na ‘Msanii Bora wa Kike’.

Drake anafuatilia kwa karibu akiwa ameteuliwa katika vipengele nane, vikiwemo ‘Msanii Bora’ na ‘Msanii Bora wa Top Billboard 200’.

Kendrick Lamar pia yupo katika vipengele nane, akishindana na Metro Boomin na Future katika kategoria ya ‘Rapa Bora.

Katika muziki wa rap kwa wanawake Nick Minaj ameteuliwa mara nyingi zaidi huku GloRilla naye akiwa katika baadhi ya vipengele muhimu katika tuzo hizo na kinara mwingine SZA, akipita katika vipengele sita, kikiwemo ‘Rapa Bora wa Kike’ na ‘Msanii Bora wa Billboard 200’.

Msanii mwingine wa kike ni Beyoncé ameteuliwa kushindania kipengele cha ‘Msanii Bora wa Kike wa Ndani’ na ‘Albamu Bora ya Ndani’.

Wanamuziki wengine watakaonogesha siku hiyo ya tuzo ni pamoja na ‘The Weeknd’, ‘Brent Faiyaz’, ‘Doja Cat’ na ‘Chris Brown’.

Related Articles

Back to top button