Muziki

Lady Gaga kuja na albamu mpya Machi 2025

NEW YORK: NYOTA wa muziki wa pop Lady Gaga mwenye miaka 38 ametangaza kuachia albamu mpya ‘Mayhem’ itakayokuwa na nyimbo 14. katika albamu hiyo zimo pia nyimbo mbili zilizotoka hapo awali, ‘Die with a Smile’ na ‘Disease’.

Gaga ameeleza: “Albamu yangu mpya ilianza kipindi ambacho nilikuwa na hofu ya kurudi kwenye muziki.”

Gaga bado hajatoa majina ya nyimbo zinazopatikana katika albamu hiyo lakini nyimbo mbili ‘Die with a Smile’ na ‘Disease’ zimeachiwa huku wimbo wa tatu ukitarajiwa kuachiwa wakati wa Tuzo za Grammy za Februari 2.

Mwimbaji huyo mzaliwa wa New York nchini Marekani amekiri kwamba: “Nataka sana kuwa sauti inayostahili kuwa sehemu ya jamii yetu katika albamu yangu hiyo mpya.”

Licha ya lkuachia albamu hiyo Lady Gaga amefafanua namna anavyotamani kuwanziaha familia akiwa na miaka 38 pamoja na mchumba wake Michael.

Mwimbaji huyo anayetamba na kibao cha ‘Poker Face’ alichumbiwa mwaka jana: “Nina furaha sana kuwa katika mapenzi na ninafurahi sana kuwa na familia, kwa hivyo hiyo ni namba moja kwangu lakini pia, ninaamini sana uwezo wa kukua kama binadamu anayependa kuwa na familia kwa sasa.”

Related Articles

Back to top button