Ligi Kuu

Masau Bwire:Kagera Sugar sio ya kubezwa

DAR ES SALAAM: OFISA Habari na Mawasiliano wa JKT Tanzania, Masau Bwire, amesema wanatarajia kukutana na upinzani mkali katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar, akieleza kuwa mabadiliko yaliyofanywa na timu hiyo yameongeza ushindani wake.

Bwire amesema wapinzani wao wameonesha uwezo katika michezo ya hivi karibuni, ikiwemo ushindi dhidi ya Mbeya City na sare dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo alioutaja kuwa mgumu.

“Tunakwenda kucheza na timu yenye uwezo na ushindani. Ni moja ya timu ambazo zimefanya mabadiliko makubwa, wamecheza na Mbeya City wakashinda na wametoka kupata sare dhidi ya Polisi katika mchezo uliokuwa mgumu,” amesema Bwire.

Amesema pamoja na ugumu unaotarajiwa, timu yao ina benchi la ufundi linaloweza kuchambua wapinzani na kuandaa mbinu za kukabiliana nao.

Bwire amemtaja kocha Ahmed Ally kuwa na uwezo wa kusoma mchezo wa wapinzani, huku akiendelea kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ili kuimarisha kikosi kabla ya mchezo huo.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 24, 2026, katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button