Ligi Daraja La Kwanza

Unashaanga hachezi vizuri kumbe kawekwa kwenye kibuyu

MGANGA wa jadi kutoka Ghana, Nana Kwaku Bonsam, amedai kuwa alitumia nguvu za kiroho kumzuia mshambuliaji wa England, Harry Kane, kufanya vizuri katika mchezo wa Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Ghana.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Bonsam alieleza kuwa alikuwa akifanya “kazi ya kiroho” kabla ya mechi hiyo kwa lengo la kumdhibiti Kane na kuisaidia Ghana kupata matokeo chanya.
Alidai kuwa juhudi hizo zilifanikiwa kwa mujibu wake, akisema Kane hakuweza kuonesha kiwango chake cha kawaida uwanjani kutokana na athari za kile alichokiita nguvu za kiroho.
Kauli hiyo imezua mijadala mikubwa mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wameichukulia kama sehemu ya utani wa soka na nyingine wakijadili nafasi ya imani za jadi na ushirikina katika michezo ya kisasa.
Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha madai hayo, na wengi katika ulimwengu wa soka huyaona kama maneno ya burudani zaidi kuliko ukweli wa kimchezo.

Related Articles

Back to top button