Kane mahistoria

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Harry Kane ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza Mwingereza kufikisha idadi ya mabao 10 kwenye michuano ya ulaya katika msimu mmoja huku Bayern wakisonga mbele baada ya kuichabanga Bayer Leverkusen jumla ya mabao 5-0.
Bao la mshambuliaji huyo la dakika ya 52 lilikuwa la 10 kwenye michuano hiyo msimu huu akiwa ni Mwingereza pekee kufikisha idadi hiyo ya mabao ndani ya msimu mmoja katika historia ya michuano hiyo.
Kabla yake Mwingereza aliyefunga mabao mengi kwenye msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya alikuwa Raheem Sterling aliyekuwa na mabao 6 msimu wa 2019/20 wakati huo akiwa Manchester City.
Bayern walikuwa na kibarua chepesi cha kushikilia uongozi wao wa mabao 3-0 walioupata nyumbani Allianz Arena wiki iliyopita na vijana hao wa Vincent Kompany kuendeleza ubabe Leverkusen.
Leverkusen ambao waliingia kwa kushambulia zaidi kipindi cha pili lakini walikuwa Bayern waliomaliza mchezo baada ya mshambuliaji wa Leverkusen Patrik Schick kuondosha vibaya free-kick ya Joshua Kimmich kisha mpira kutua kwenye miguu ya Harry Kane alitoboa jahazi la Leverkusen dakika ya 52.
Bayern sasa watakutana na Inter Milan kwenye robo fainali ya UEFA Champions League baada ya mabingwa hao wa Serie A kuwafumua Feyenoord kwa jumla ya mabao ya 4-1. Mechi ya mkondo wa kwanza inatarajiwa kupigwa kati ya April 7 au 8 na mkondo wa pili wiki moja baadae.