Ligi Daraja La Kwanza

Master Rim FC kubeba wachezaji Zambia, DR Congo

MMILIKI wa timu ya Master Rim FC, Kassim Ahmed amesema katika kuboresha upana wa kikosi hicho wamepanga kuleta wachezaji wapya kutoka mataifa ya Zambia na DR Congo.

Akizungumza na SpotiLEO, Ahmed amesema mipango hiyo itaanza mara baada ya kukamilisha taratibu za usajili kwa ajili ya kuanza kucheza Ligi Daraja la Tatu.

“Kabisa tena na pia tumeshaongea na wadhamini mbalimbali kwa mfano kama kampuni za simu kama mbili zote hizo zipo tayari kutuunga mkono,” amesema Ahmed.

Amesema wamepata funzo na namna ya kuboresha kikosi hicho mara baada ya kushiriki mashindano ya Ndondo Cup na Ramadhan Cup msimu uliopita.

Timu hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili kushiriki Ligi Daraja la Tatu za mikoa

Related Articles

Back to top button