Filamu

Muongoza filamu atunukiwa Tuzo ya Mafanikio ya Maisha

MOMBASA: MTAYARISHAJI na mwongozaji mkongwe wa filamu kutoka Kenya, Judy Kibinge, ameendelea kuandika historia baada ya kutunukiwa Tuzo ya Mafanikio ya Maisha (Lifetime Achievement Award) katika tamasha la tano la Pridelands Wildlife Film Festival linaloendelea jijini Mombasa.

Tuzo hiyo imekuja kwa heshima kwa mchango wake mkubwa katika kukuza tasnia ya filamu Afrika pamoja na juhudi zake za kuwainua watengenezaji wa filamu huru kupitia Docubox, mfuko wa kwanza wa kusaidia filamu za makala ulioanzishwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Kibinge alisema heshima hiyo ina uzito wa kipekee kwake kwa sababu inatoka kwenye taasisi inayopigania simulizi za Waafrika kusimuliwa na Waafrika wenyewe.

Judy ameendelea kuwa mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa katika sekta ya ubunifu barani Afrika, huku kazi zake zikiheshimiwa kimataifa.

Mwaka 2017 aliingia kwenye kundi la wapiga kura wa tuzo za Oscars, hatua iliyothibitisha hadhi yake katika ulimwengu wa filamu.

Waandaaji wa tamasha hilo wamemtaja Kibinge kama kinara aliyefungua milango kwa kizazi kipya cha watengenezaji wa filamu na kusaidia sauti za Afrika kusikika duniani kote.

Related Articles

Back to top button