Tennis

Lebron James aweka kitendawili NBA

LOS ANGELES: NYOTA wa Los Angeles Lakers, LeBron James amesema bado hajafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake wa kucheza NBA baada ya timu yake kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya Kanda ya Magharibi dhidi ya Oklahoma City Thunder.

Thunder waliibuka na ushindi wa pointi 115-110 na kukamilisha ushindi wa jumla wa 4-0 katika mfululizo huo wa play-off, huku LeBron akifunga pointi 24 na kuongoza kwa rebounds 12.

Baada ya mchezo huo, LeBron mwenye miaka 41 amesema bado anahitaji muda wa kutafakari pamoja na familia yake kabla ya kufanya maamuzi kuhusu maisha yake ya baadaye kwenye mchezo huo.

Mchezaji huyo aliyemaliza msimu wake wa 23 ndani ya NBA amesema hafikirii kama msimu huu ulikuwa wa kukatisha tamaa licha ya Lakers kushindwa kutinga hatua inayofuata.

LeBron pia ameeleza kuwa kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka la kikapu alilazimika kucheza kama chaguo la tatu ndani ya timu, nyuma ya Luka Doncic na Austin Reaves, lakini bado aliweza kuisaidia timu katika mazingira magumu yaliyokumba kikosi hicho kutokana na majeraha.

Katika play-off za msimu huu, LeBron alimaliza akiwa na wastani wa pointi 23.2, assists 7.3 na rebounds 6.7 kwa kila mchezo.

 

Related Articles

Back to top button