Tennis

Kisa goti Djokovic kuukosa utamu wa French Open

PARIS: Namba moja wa tenis duniani na bingwa mara 24 wa Grand Slam, Novak Djokovic amejiondoa kwenye michuano ya French Open kabla ya robo fainali yake dhidi ya Casper Ruud kutokana na jeraha la goti alilolipata katika raundi ya awali.

Djokovic alitarajiwa kucheza na Ruud Jumatano kuwania nafasi ya nne bora katika mchezo wa fainali ya mwaka jana huko Roland Garros Djokovic akimshinda Ruud kwa seti mfululizo.

“Nina huzuni sana kutangaza kwamba lazima nijiondoe kutoka kwa Roland Garros,”  aliandika Djokovic kwenye kurasa za mitandao yake ya kijamii.

“Nilicheza kwa moyo wangu na kujitolea katika mechi ya jana na kwa bahati mbaya, kutokana na kupasuka kwa ‘meniscus’ kwenye goti langu la kulia, mimi na timu yangu tulilazimika kufanya uamuzi mgumu baada ya kutafakari na kushauriana kwa kina.” Alieleza Djokovic.

Waandaaji wa mashindano hayo walitangaza kujiondoa kwake wakisema uchunguzi wa MRI ufanyike mapema ili ubainishe ukubwa kamili wa jeraha hilo kasha wakamuombea Djokovic apone haraka ili arejee katika mchezo huo

Related Articles

Back to top button