La Liga

Barca waisogelea taji, Real Madrid waichelewesha sherehe

MADRID:KLABU ya Real Madrid imeilazimisha Barcelona kusubiri kutwaa ubingwa wa La Liga baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Espanyol.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa RCDE, nyota wa Madrid, Vinícius Júnior, aliibuka shujaa kwa kufunga mabao yote mawili kipindi cha pili dakika ya 55 na 66, akimalizia pasi za Gonzalo García na Jude Bellingham.

Ushindi huo unaifanya Barcelona kusubiri kuthibitisha ubingwa, huku sasa ikiwa na nafasi ya kipekee kufanya hivyo katika dabi ya kihistoria ya El Clasico itakayopigwa wikiendi ijayo.

Barcelona wanahitaji sare pekee ili kutwaa taji hilo mbele ya wapinzani wao wakubwa, jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya ligi hiyo ya zaidi ya miaka 90.

Endapo watafanikiwa, Barcelona wanaweza kuweka rekodi mpya, ikiwemo kumaliza msimu wakiwa na alama 100 pamoja na ushindi mwingi zaidi, huku pia wakivunja rekodi ya tofauti kubwa ya pointi dhidi ya mshindani wao wa karibu.

Kwa upande wa Real Madrid, ushindi huo unawaweka hai kwa heshima ya kumaliza msimu kwa nguvu, ingawa wanakabiliwa na hatari ya kumaliza bila taji kwa msimu wa pili ndani ya miaka michache.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button