Ligi Kuu

Barker: Simba ni ngumu kufungwa

ARUSHA: KOCHA Mkuu wa Simba, Steven Barker amesema kikosi chake kinapaswa kuendelea kuwa imara kwa dakika zote 90 za mchezo ili kuepuka kuruhusu mabao ya kizembe, kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya TRA utakaochezwa kesho mkoani Arusha.

Akizngumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Barker amesema moja ya maeneo muhimu ambayo benchi la ufundi linaendelea kulifanyia kazi ni uimara wa safu ya ulinzi, akieleza kuwa mechi nyingi huamuliwa katika dakika za mwisho, jambo linalohitaji umakini mkubwa kwa wachezaji wake.

Amesema tangu alipojiunga na Simba, timu imekuwa ikionesha kiwango kizuri katika eneo la kujilinda, lakini bado kuna umuhimu wa kuendelea kuboresha zaidi ili kuifanya Simba kuwa timu ngumu kufungwa na inayowapa wapinzani nafasi chache za kushambulia.

“Siwezi kuzungumzia sana sehemu ya mwanzo wa msimu, lakini tangu nilipokuja hapa nafikiri tumefungwa mabao matatu tu. Hilo ni eneo muhimu sana kwa sababu mechi nyingi za soka huamuliwa katika hatua za mwisho za mchezo,” amesema Barker.

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa timu yake kuanza mchezo kwa nguvu, lakini jambo la msingi zaidi ni kuhakikisha wanaendelea kuwa na umakini, nidhamu na mpangilio mzuri hadi dakika ya mwisho.

Kocha huyo amesema kuwa Simba inapaswa kudumisha umakini katika kila kipengele cha mchezo ili kumaliza mechi kwa nguvu na kuepuka kufungwa katika nyakati muhimu

Mchezo huo dhidi ya TRA awali uliahirishwa kutokana na mvua kubwa mkoani humo na sasa wanarudi tena.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button