Ligi Kuu

Simba wanasajili, Yanga wanalumbana

Awesu asaini kibabe Simba

Wakati leo Yanga wakilazimika kutoka hadharani na kutolea ufafanuzi sakata linaloendelea kwenye timu hiyo, wapinzani wao wakuu Simba wameendelea kuimarisha timu yao.
Leo Simba imemtambulisha rasmi aliyekuwa kiungo wa KMC FC, Awesu Awesu kwa mkataba wa miaka miwili.
Uwesu ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakiwindwa na Yanga, kutaka huduma ya kiungo huyo baada ya msemaji wa klabu hiyo kusema kuwa akipewa nafasi ya kupendekeza viungo wazawa jina na nyota huyo lingekuwepo.
Simba wamefanikiwa kuinasa saini ya Awesu baada ya kuwepo kwa mazungumzo baina ya klabu ya Simba na KMC FC kwa ajili ya kufanya biashara ya kumnunua nyota huyo.
Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kiungo huyo ni sehemu ya mipango ya timu hiyo katika maboresho ya timu yao kwa msimu mpya.
 
“Awesu amejiunga nasi akitokea KMC FC , aliyodumu nayo miaka mitatu, mchezaji mzoefu kwenye ligi anaweza kumudu nafasi ya kiungo, ushambuliaji na winga zote na amewahi kucheza kama kiungo mkabaji.
Muda wowote anatarajia kwenda nchini Misri kuungana na wachezaji wenzake waliopo kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano,” amesema Ahmed.

Related Articles

Back to top button