Burudani

Utabiri washindi wa Oscars 2026 waanza kutikisa Hollywood

Michael B Jordan ndani

LOS ANGELES: Wakati maandalizi ya tuzo za Academy Awards za mwaka 2026 yakifikia kilele, wachambuzi wa filamu wameanza kutoa utabiri wa nani anaweza kuibuka mshindi.

Filamu ya One Battle After Another inayoongozwa na Paul Thomas Anderson inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya filamu bora ikiwa na takribani asilimia 60.

Katika kipengele cha muigizaji bora wa kiume, nyota Michael B. Jordan anaonekana kuongoza kwa silimia 40, akimzidi kidogo Timothée Chalamet ambaye ana asilimia 35.

Tuzo za Academy Awards maarufu tuzo za Oscars kwa mwaka 2026 zinatarajiwa kufanyika Machi 15, 2026 katika Ukumbi wa Dolby Theatre, Hollywood, katika jiji la Los Angeles nchini Marekani.

Tuzo hizo ni toleo la 98 la tuzo za Oscars, zinazotolewa na kampuni ya Academy of Motion Picture Arts and Sciences kwa ajili ya kutambua filamu bora zilizotolewa mwaka 2025 na hizi ndizo tuzo kubwa zaidi duniani katika tasnia ya filamu.

Filamu zote zilizopokelewa zimewekwa katika vipengele 24. Kwa mwaka huu kutakuwa na zurua jekundu ambapo mtangazaji wa sherehe hizo atakuwa mchekeshaji Conan O’Brien.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button