Burudani
Watunzaji waonywa udhalilishaji kwa wanenguaji
RAIS wa Madansa nchini, Hassan Mussa maarufu ‘Super Nyamwela’ amewataka mashabiki wa muziki huo kuacha tabia ya kuwadhalilisha wanenguaji wa kike wanapokuwa majukwaani.
Super Nyamwela ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi ya Ubuntu inayopiga muziki wa asili alisema wameamua kuyatolea kauli matukio hayo ya kuwashika wanenguaji hao baadhi ya sehemu zao za mwili kwa kuwa yamekuwa na udhalilishaji.
“Hatukatazi kutunzwa ila hatutaki dada zetu wawekewe fedha kwenye sehemu za miili yao sababu huo ni udhalilishaji na tutawachukulia hatua nashabiki wa aina hiyo,” alisema Super Nyamwela
Super Nyamwela pia amewataka wanenguaji wa muziki wa aina yoyote wajiunge na chama chao ili wapate fursa mbalimbali ikiwemo bima ya afya.