Ligi Kuu

Meneja Uwanja wa Mkwakwani kusimamishwa kazi

TANGA: Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga, Rajabu Abdallah ameiagiza kamati ya siasa mkoa kumsimamisha kazi meneja wa uwanja wa CCM Mkwakwani kwa madai ya kushindwa kusimamia uwanja huo.

Maagizo hayo ameyatoa wakati wa ziara yake ya kutembelea kukagua maendeleo ya uwanja huo Jumatano Machi 11,2026 ambapo ametoa  mwezi mmoja kuhakikisha uwanja huo umefungwa viti na kufanyiwa usafi.

Hata hivyo Meneja wa Uwanja wa Mkwakani Akida Machai akaeleza hatua mbalimbali ambazo uwanja huo umefikia.

Mwenyekiti wa CCM ameonyesha dhamira ya dhati ya kuungamkono mpira wa miguu ambapo tayari alishachangia sh mil 50 kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo.

Related Articles

Back to top button