Muziki
Shakira anogewa ziara ya India

INDIA: Mwanamuziki maarufu duniani Shakira ameongeza tamasha jingine katika ziara yake ya muziki nchini India kufuatia mahitaji makubwa ya tiketi kutoka kwa mashabiki.
Kwa mujibu wa waandaaji, tamasha jipya litafanyika Aprili 11 katika uwanja wa Mahalaxmi Racecourse jijini Mumbai, siku moja baada ya tamasha la kwanza lililopangwa Aprili 10 katika eneo hilo hilo.
Mbali na Mumbai, Shakira pia anatarajiwa kufanya tamasha jingine Aprili 15 katika mji wa Delhi. Waandaaji wanasema ongezeko hilo la maonesho limetokana na kile walichokiita mahitaji yasiyo ya kawaida ya uuzaji wa tiketi.




