Muziki

Dr Dre kushiriki Olimpiki 2028 Marekani

LOS ANGELES: MSANII wa muandaaji wa muziki nchini Marekani, Andre Young ‘Dr Dre’ huenda akaiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika Los Angeles mwaka 2028 katika mchezo wa kurusha mishale.

Taarifa iliyochapishwa na ‘Billboard’ imenukuu mtandao wa ‘Entertainment Tonight’ kuwa historia ya Dr Dre kurusha mishale inarudi kipindi akiwa shule hata hivyo ameendelea kuboresha na kufanya mazoezi ya kulenga shabaha.

“Nitajaribu Olimpiki 2028” alisema na kuongeza kuwa: “Kwa kweli nilianza kucheza mishale katika kiwango cha juu, nilisikia kufuzu kwa Olimpiki ni futi 77 na ninafanya mazoezi ya futi 90.”

Dr Dre aliendelea kusema: Nadhani suala hilo linavutia sana hasa kuwa pale Los Angeles na kushinda medali…nahisi kama naweza kufanya kitu.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button