Nyumbani

Khalid Aucho afunguka Sakata la kufungiwa

DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Singida Black Stars, Khalid Aucho, amevunja ukimya kufuatia uamuzi wa klabu yake kumfungia kwa muda wa miezi mitatu kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Kupitia ujumbe wake, Aucho ameeleza kuwa katika maisha yake yote ya soka amekuwa akijiheshimu na kuzingatia taaluma, akidai hajawahi kuhusishwa na tukio lolote la utovu wa nidhamu.

“Nimekuwa nikijibeba kwa weledi katika maisha yangu yote ya soka, nikiwakilisha kila klabu kwa heshima na nidhamu. Katika miaka yote niliyocheza mpira, sijawahi kuhusishwa na kesi yoyote ya utovu wa nidhamu kwa sababu ninaelewa wajibu unaokuja na kuwa mchezaji wa kulipwa,” ameeleza Aucho.

Nyota huyo raia wa Uganda ameongeza kuwa ana imani hali hiyo itapita na kurejea katika ubora wake, huku akitoa shukrani kwa mashabiki wanaoendelea kumuunga mkono katika kipindi hiki kigumu.

“Kwa mashabiki wangu wapendwa ambao mmekuwa nami wakati wote, hali hii itapita. Asanteni kwa msaada wenu endelevu,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button