Nyumbani

Coastal Union si Kinyonge hata kidogo

TANGA: UONGOZI wa Coastal Union umeweka wazi mipango ya usajili na kuangalia zaidi safu ya ushambuliaji kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongwa na Kocha David Ouma kueleza maeneo ya kufanyiwa maboresho kwa msimu ujao wa mashindano ya kimataifa.

Akizungumza na Spotileo, Ofisa habari wa Coasta Union, Abbas Elsabri amesema Kocha Ouma amekabidhi ripoti ya tathimini ya msimu huu, wanaimarisha safu ya ushambuliaji baada ya kukosena mchezaji wa timu hiyo katika orodha ya ufungaji mzimu huu.

Amesema mchakato wa usajili umeanza mapema kwa kuangalia sifa na uwezo wa mshambuliaji anayemtaka, wanaangalia timu zote za ndani zinazoshiriki Ligi Kuu iwe Namungo FC, Azam FC, Simba na Yanga.

“Kocha Ouma ameshatoa maagizo ya watu anaowataka kuwasajili, kamati ya usajili wanafanyia kazi, ripoti hiyo kwa kuwangalia maeneo yote kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha timu yetu ukizingatia safari hii tunaenda kucheza kombe la Shirikisho Afrika,” amesema Abbas.

Ameongeza kuwa mbali na kuangalia safu ya ushambuliaji wanaongeza nguvu beki safu ya ulinzi baada ya beki wao Lameck Lawi kutokuwepo kwa msimu ujao ndani ya kikosi cha Coastal Union.

Kuhusu kurejeshwa kwa Juma Mgunda, amesema licha ya kocha huyo kuwa ni mwana Coastal Union hawawezi kumuondoa Simba kwa sababu ya mkataba wake ndani ya klabu hiyo.

“Unajua tukumbuke kuwa kocha wetu Ouma ndio amefanikisha Coastal Union kucheza michuano ya kimataifa hii ni baada ya miaka 35 kupita, tukimuacha kocha huyo hatutatenda haki kwake na tunaimani naye,” amesema Ofisa habari huyo.

Coastal Union ni miongoni mwa timu za nne Tanzania zitakazoenda kuwakilisha nchini katika mashindano ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya kumaliza nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Related Articles

Back to top button