Ligi Kuu

Sowah bado hakijaeleweka Simba

DODOMA: MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema mshambuliaji Jonathan Sowah yupo nje ya kikosi na hatma yake ya kusafiri na timu kuelekea Zanzibar bado haijafahamika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Ally ameeleza kuwa mara baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Sowah alirudishwa kambini lakini siku iliyofuata akaondoka na kurejea Dar es Salaam, hali iliyoibua sintofahamu ndani ya kikosi hicho.

Amesisitiza kuwa sababu za nyota huyo kuwa nje ya timu zitawekwa wazi na uongozi wa klabu pindi utakapotoa taarifa rasmi.

“Sowah tulimtoa kambini na kumrejesha mara baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, siku iliyofuata akaondoka kambini na kurejea Dar es Salaam. Sijui kama tutakuwa naye Zanzibar. Yupo nje ya kikosi toka juzi, nini sababu mpaka pale klabu itakapotoa taarifa,” amesema Ahmed Ally.

Kutokuwepo kwa mshambuliaji huyo kunazua maswali kwa mashabiki wa Simba, hasa katika kipindi hiki ambacho timu inaendelea na maandalizi ya mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Yanga utakaochezwa Jumapili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button