Nyumbani

Yanga yaenda Zanzibar kwa Maandalizi ya kuivaa JS Kabylie

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha Yanga SC leo kimewasili Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya mwisho kuelekea mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Kabylie ya Algeria.

Mchezo huo muhimu utapigwa Jumapili katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar, ukiwa ni wa kuamua hatma ya Wananchi katika michuano hiyo ya ngazi ya juu barani Afrika.

Yanga inaingia katika pambano hilo ikiwa kwenye presha ya matokeo baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya FAR Rabat kwa bao 1-0, hali iliyofanya safari yao ya kufuzu kuwa ngumu na kutegemea mahesabu.

Hatma yao inategemea pia matokeo ya mchezo mwingine wa kundi hilo. Ili kufuzu, Yanga inalazimika kuibuka na ushindi wa angalau mabao mawili dhidi ya JS Kabylie, sambamba na kumuombea Al Ahly ya Misri iwafunge FAR Rabat kwa tofauti ya mabao mawili au zaidi.

Hali hiyo inaifanya mechi ya Jumapili kuwa mtihani mkubwa kwa Yanga, lakini benchi la ufundi pamoja na wachezaji wanaamini bado nafasi ipo iwapo watatumia vyema faida ya kucheza nyumbani.

Related Articles

Back to top button