Mastaa
TANZIA: Mama mzazi wa msanii Chid Benz afariki dunia

DAR ES SALAAM:MAMA mzazi wa msanii wa Hip Hop nchini Tanzania, Rashid Abdallah maarufu kama Chid Benz, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Februari 11, 2026.
Taarifa zilizothibitishwa na familia zinaeleza kuwa marehemu, Bi. Hawa, amefariki na kwa sasa msiba upo nyumbani kwa familia eneo la Chanika, jijini Dar es Salaam.
Familia imesema kuwa taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi zitatolewa baadaye.
Kifo hicho kimeacha simanzi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa muziki nchini, huku wengi wakituma salamu za pole kwa msanii Chid Benz na familia yake kwa ujumla.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
SpotiLeo tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliofikwa na msiba huu.




