Mastaa

Aika awachana wanawake wasio wavumilivu

DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa rege aina ya dancehall Aika Marealle ‘Aika’ amesema warembo wengi wanapoteza miaka mingi ya kururahia na kujenga uhusiano kwasababu wameweka matarajio makubwa kwa wanaume.

Kupitia akaunti yake ya kijamii, nyota huyo amesema wanaume ni watu wenye hisia, hulia sio wakamilifu na kwamba hawakuzaliwa na maarifa yote ya kuweza kutimiza matamanio yao.

“Msipoteze muda wenu mkitafuta mwanadamu mkamilifu atakayewaletea chai kitandani, maua kazini au kuwa‘suprise’ kwa likizo.Badala yake chukueni muda kujengana, kusaidiana, kufundishana, uhusiano hujengwa kama nyumba sio muujiza,”amesema.

Aika amekuwa kwenye mahusiano na msanii mwenzake Emmanuel Mkono ‘Nahreel’, kwa zaidi ya miaka 15 na walikutana wakiwa Chuo mwaka wa kwanza nchini India mwaka 2008 na hadi sasa wanaishi kama mke na mume wakiwa bado hawajafunga ndoa ila wamebarikiwa kupata watoto wawili.

Wote wawili wameunda kundi lao la muziki linaloitwa Navykenzo wakifanya shughuli zao za muziki pamoja.

Related Articles

Back to top button