Muziki

Man Fongo kutetea wanawake, watoto

ZANZIBAR: MSANII wa singeli,Man Fongo ameweka wazi kuwa anaandaa nyimbo zenye jumbe maalumu za kutetea haki za Wanawake na Watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Man Fongo amesema hayo katika mjadala ulioandaliwa na UNICEF kwa kushirikiana na Sauti za Busara, uliojikita katika namna wasanii wanavyoweza kutumia sauti na ushawishi wao kukemea ukatili na kutetea haki za wanawake na watoto.

Mjadala huo uliwakutanisha wasanii, wadau wa sanaa na wataalamu wa ulinzi wa watoto kutoka UNICEF, kwa lengo la kuhimiza utengenezaji wa kazi zitakazoishi vizazi na vizazi.

Wasanii na waandishi mbalimbali wametoa maoni yao katika mjadala huo na namna ya kusaidia wanawake na Watoto kutimiza ndoto zao.

Related Articles

Back to top button