Mashabiki wa Chris Brown wacharuka

MAREKANI: BAADA ya Msanii kutoka nchini Marekani Chris Brown kutajwa kama msanii aliyeshika nafasi ya 18 kwa wasanii wakubwa zaidi wa karne ya 21 na Jarida la Billboard, Mashabiki wamepinga taarifa ya jarida hilo na kudai kuwa anastahili kupewa nafasi ya tatu.
Hata hivyo, mashabiki wake wameshikilia msimamo kwamba staa huyo anastahili nafasi ya juu zaidi kwenye orodha hiyo, inayoongozwa na Taylor Swift na wengine wakimpongeza.
Kwa mujibu wa baadhi ya maoni ya mashabiki wake walisema “Anastahili kuwa top 10.” – @charleymabr3
“18!? Siwezi kuichukulia orodha hii kwa uzito.” – @Zigggy21″Nafikiri nafasi hii imeshuka kutokana na tukio la Rihanna.” @Oluwatrillions, “Anapaswa kuwa #3, si 18!” – @coolboi_real
Baadhi ya mashabiki walihisi kwamba mchango wa Chris Brown kwenye muziki ungempa nafasi ya juu zaidi, hasa kutokana na mafanikio yake kwenye chati za Billboard na kazi yake isiyo na kikomo.
Wengine walihusisha nafasi hiyo na historia ya maisha yake binafsi, wakisema kuwa inaweza kuwa imeathiri jinsi anavyoonekana.
Chris Brown, ambaye amekuwa na albamu kadhaa zilizoongoza chati na nyimbo maarufu duniani, anaendelea kuwa mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa kwenye muziki wa R&B na pop, licha ya mijadala mingi ya kubaguliwa.
Mashabiki wengi wanaamini kuwa mchango wake unapaswa kuzingatiwa zaidi, huku wengine wakimpongeza kwa kutambuliwa kwenye orodha ya wasanii wakubwa wa wakati huu.