Muziki

Marioo apongeza upendo wa mashabiki

'Oluwa' yapata mapokezi chanya mtandaoni

DAR ES SALAAM: MSANII Omary Mwanga maarufu kama Marioo amewashukuru mashabiki wake kwa upendo mkubwa wanaoendelea kumuonyesha, kufuatia mapokezi mazuri ya kazi yake mpya ya muziki.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Marioo amendika:
“Kusema ukweli mko na upendo mkubwa sana. Last night hata hao Wasauzi wenyewe walishangaa hayo mawe yalivyokuwa yanalia,” ameandika Marioo.

Hatua hiyo imekuja huku ikionekana mashabiki wake wakiendelea kumuunga mkono, wakidhihirisha imani yao kwake kupitia mapokezi chanya ya wimbo wake mpya ‘Oluwa’. Wimbo huo umeanza kwa kasi kubwa, ukipata mafanikio mazuri kwenye mtandao wa YouTube ikilinganishwa na kazi za wasanii wengine kwa kipindi hicho.

Ndani ya dakika 14 tangu kuachiwa kwake, “Oluwa” ulikuwa tayari umekusanya watazamaji zaidi ya 9,000, jambo linaloashiria mwitikio chanya na kurejea kwa nguvu kwa Marioo kwenye ramani ya muziki.

Mashabiki na wadau wa muziki wanaendelea kufuatilia mwenendo wa wimbo huo, wakiamini kuwa utaendelea kufanya vizuri zaidi kadri siku zinavyosonga.

Related Articles

Back to top button