Muziki

Tamasha la Burna Boy Kenya lahofiwa kuleta foleni

KENYA: WAKAZI wa Nairobi na madereva wa magari wameshauriwa kuchukua hatua za njia za kupita Jumamosi, Machi 1 kwa kuwa baadhi ya Barabara zinatarajiwa kufungwa kutokana na tamasha aliloalikwa mwanamuziki wa Nigeria Burna Boy la MadfunXperience litakalofanyika bustani ya Uhuru Gardens, karibu na Barabara ya Lang’ata.

Tukio hilo linalotarajiwa kuvuta umati mkubwa wa watu, linadaiwa litaathiri barabara muhimu ya Lang’ata, Likoni, na kiungo kutoka Southern Bypass hadi Likoni kupitia Uwanja wa Carnivore.

Msongamano wa magari unatarajiwa kutokea kimsingi mwanzoni na mwisho wa tukio, wahudhuriaji wanapowasili na kuondoka katika tamasha hilo litakalowajumuisha wasanii wa Nigeria, Afrika Kusini na Kenya.

Mamlaka ya usalama Barabarani nchini humo imewataka madereva kupanga safari zao ipasavyo na kuzingatia njia mbadala ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Uongozi wa tamasha hilo umeshauri baadhi ya wahudhuriaji wa tamasha hilo kutumia usafiri wa umma kama vile Uber, matatu au pikipiki (boda boda) kufika katika tamasha hilo ili kupunguza msongamano na kuhakikisha mtiririko mzuri wa trafiki katika eneo hilo.

Zaidi ya hayo, wahudhuriaji wote wanahimizwa kuzingatia ishara na kufuata maagizo kutoka kwa mamlaka ya trafiki na waandaaji wa hafla ili kuhakikisha hali salama inakuwa ya kuridhisha kwa kila mtu na si kukera.

Related Articles

Back to top button