Filamu ya Leonardo DiCaprio ‘yaoga’ tuzo

LOS ANGELES: FILAMU ya Paul Thomas Anderson, ‘One Battle After Another’, imeshinda tuzo moja pekee na kuibuka mshindi wa jumla kwa kutwaa tuzo ya ‘Best Feature’ licha ya kugombea vipengere sita.
Wakati wa kupokea tuzo hiyo, Anderson alikiri kwa unyenyekevu kwamba hakutegemea kupata tuzo hiyo, ambayo muhusika mkuu ni Leonardo DiCaprio, “Sikutarajia hili,”.
Tuazo hiyo aliielekeza kwa mke wake, Maya Rudolph, kwa kumbukumbu ya miaka 24 ya ndoa yao, akisema, “Miaka 24 iliyopita nilikutana na mwanamke aliyenifanya kuwa mzalishaji bora wa filamu.”
Wengine walioibuka na tuzo usiku hu oni Pamoja na mcheza filamu maarufu kutoka Iran, Jafar Panahi, aliyeibuka nyota wa usiku huo kwa filamu yake It Was Just an Accident’.
Filamu hii ilishinda tuzo zote tatu zilizokuwa zikimshindania ikiwemo tuzo ya ‘Filamu ndefu ya Kimataifa’, ‘Filamu yenye uhalisia’, na ‘Muongozaji bora’.
Hii ilitokea muda mfupi tu baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela nchini Iran, ingawa alihudhuria hakuhukumiwa rasmi kwa kuikana kuhudhuria mahakamani.
Katika hotuba yake, Panahi alitumia tuzo hizi kuzipeleka kwa waandaaji wa filamu huru nchini Iran na duniani kote.
“Kwa waandaaji wa filamu huru Iran na duniani kote… ambao wanachukua hatari zote kwa imani yao kwa ukweli na utu.”, “Niko hapa usiku huu,” akionyesha shukrani kwa kuendelea na kazi yake, licha ya changamoto.
Wengine walioshinda ni Filamu ya ‘My Father’s Shadow’ ilishinda tuzo zote mbili zilizokuwa zikimshindania:
Tamasha hili limeonesha wazi mafanikio makubwa ya filamu na waandaaji wa filamu, huku likimupongeza pia watu waliotangaza na kuendeleza ubunifu na hamasa katika tasnia ya filamu duniani kote.




