Mastaa

Paula: Wiki nzima ni ya kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa

DAR ES SALAAM: Paul Kajala amesema wiki hii yote ni maalumu kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, huku akieleza kuwa anaadhimisha hatua mpya ya maisha yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Paula aliandika: “This birthday week, I’m celebrating the woman I’m becoming,” akimaanisha kuwa anasherehekea mwanamke anayezidi kuwa kadri siku zinavyosonga.

Sambamba na ujumbe huo, Paula amechapisha picha mbalimbali zikimuonesha katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa, akionekana mwenye furaha huku akiendelea kupokea salamu na pongezi kutoka kwa mashabiki, marafiki na watu mbalimbali.

Miongoni mwa waliomtumia salamu za kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa ni mpenzi wake, msanii wa Bongo Fleva Omary Mwanga, maarufu kwa jina la Marioo, ambaye pia ni baba wa mtoto wake.

Chapisho hilo limeendelea kuvutia hisia za wafuasi wake wengi waliomtakia maisha marefu, afya njema na mafanikio zaidi katika maisha yake binafsi na safari yake ya kisanii.

Related Articles

Back to top button