Ligi KuuNyumbani

Uchovu umesababisha tupate suluhu-Minziro

Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fredy Minziro.

BAADA ya Geita Gold kulazimisha suluhu dhidi ya Coastal Union ugenini uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Geita Fredy Minziro amesema uchovu wa wachezaji wa timu yake umechangia kupata matokeo hayo.

Akizungumza na Spotileo, kocha huyo amesema uchovu huo umetokana na safari ndefu hali iliyosababisha kukosa muda wa mapumziko na kufanya maandalizi vizuri kwa ajili ya mchezo huo.

“Tulikuwa Singida kucheza na Dodoma baada ya hapo tukarudi Mwanza kabla ya kuja Tanga kwa ajili ya mchezo huu ukweli wachezaji wamecheza mfululizo na hawajapata muda wa wa kutosha kupumzika lakini hatuna namna lazima tuifuate ratiba inavyosema,” amesema Minziro.

Amesema bado hajaridhishwa na nafasi waliyopo kwenye msimamo hivyo watapambana kuhakikisha wanaimarika na kupata ushindi kwenye mechi zijazo.

Geita inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 7.

Related Articles

Back to top button