Ligi KuuNyumbani

‘Asante Sana’ Minziro

KLABU ya Tanzania Prisons imetangaza kusitisha mkataba wake na kocha Fredy Minziro.

Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Tanzania Prisons, Ajabu Kifukwe imesema uongozi wa klabu hiyo unamshukuru kwa kila kitu alichofanya katika klabu hiyo.

“Kwa manufaa makubwa ya timu uongozi umesitisha mkataba wa kocha Minziro kuanzia leo kwa makubaliano ya pande zote mbili,” imesema taarifa hiyo.

Imesema kwa kipindi hiki timu hiyo itakuwa chini ya kocha msaidizi Shabani Mtupa hadi maamuzi mingine yakapotangazwa.

Prisons inakuwa timu ya saba ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuachana na kocha wake msimu huu. Nyingine ni Simba, Ihefu, Namungo, Coastal Union, Mtibwa Sugar na Singida Fountain Gate.

Related Articles

Back to top button