EPL

Mount tena!

MANCHESTER: KOCHA mkuu wa Manchester United Ruben Amorim amesema majeraha ya hivi karibuni ya kiungo wake Mason Mount yatamsubirisha nje wiki kadhaa kabla ya nyota huyo kurejea na jezi ya klabu hiyo uwanjani.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Bournemouth Amorim amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa bado hajui ni lini kiungo huyo atakuwa fiti tena uwanjani

“Itakuwa wiki kadhaa sijui hasa muda atakaokuwa nje lakini utakuwa muda mrefu, najua ni sehemu ya mchezo na lazima tuendelee mbele” amesema Amorim

Mason Mount amekuwa akiandamwa na majeraha tangu alipotua United akicheza mechi 14 pekee za ligi kuu ya England. Msimu huu Mount amecheza dakika 243 pekee

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button